TED Talks with Swahili transcript

Niti Bhan: Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi

TEDGlobal 2017

Niti Bhan: Fursa zilizofichwa katika sekta isiyo rasmi
1,222,576 views

Niti Bhan anatafiti mikakati ya kibiashara kwa soko lisilo rasmi la Afrika: maduka madogo, wabunifu walio na ujuzi na wafanya kazi ambao ni injini isiyoonekana ambayo inafanya uchumi wa bara kusonga mbele. Inashawishi kuwaza kwamba wafanya kazi hawa ni wakwepa kodi, wahalifu -- lakini anaelezea suala hili kwamba kipande hiki ambacho kinakuza uchumi ni halali kinafaa kuwekeza. Kama tutafanya, anasema, tutatengeneza maelfu ya ajira. "Hizi ni mbegu zenye rutuba za biashara na viwanda," Bhan anasema. "Je, tunaweza kuanza kwa kutambua ujuzi huu na kazi?"

Gus Casely-Hayford: Hadithi hodari zilizoitengeneza Afrika.

TEDGlobal 2017

Gus Casely-Hayford: Hadithi hodari zilizoitengeneza Afrika.
1,248,246 views

Katika ufutaji mkubwa wa historia, hata dola inaweza kusahaulika. Katika hotuba hii pana, Gus Casely-Hayford anaelezea hadithi halisi za Afrika ambazo mara nyingi huwa haziandikwi, zimepotea, hazijasambazwa. Akisafiri kuelekea Zimbabwe kuu, jiji kongwe ambalo chimbuko lake la kustaajabisha na usanifu majengo wa hali ya juu unawaumiza vichwa wana-akiolojia. Au nyakati za Mansa Musa, mtawala wa dola ya Mali ambaye utajiri wake mkubwa ulijenga maktaba za Timbuktu. Na pia fikiri mafunzo yapi mengine ya historia tunaweza kuyadharau kwa bahati mbaya.

Nikki Webber Allen: Usitaabike na msongo wa mawazo katika ukimya.

TED Residency

Nikki Webber Allen: Usitaabike na msongo wa mawazo katika ukimya.
2,292,266 views

Kuwa na hisia si dalili ya udhaifu -- humaanisha kwamba sisi ni binadamu, anasema mtayarishaji vipindi na mwanaharakati Nikki Webber Allen. Hata baada ya kugundulika na ugonjwa wa msongo wa mawazo na hofu, alijisikia aibu kumwambia mtu yoyote, aliweka hali yake katika usiri mpaka pale msiba wa mtu wa karibu katika familia yake ulipotokea, kutokana na hali kama yake. Katika mjadala huu muhimu kuhusu afya ya akili, anaongelea wazi kuhusu hangaiko lake -- na kwanini jamii ya watu wasio wazungu ina ulazimu wa kuondokana na unyanyapaa ambao huepelekea watu kuwaza msongo wa mawazo ni udhaifu na kuwatenga walio na hangaiko hilo katika kupata msaada.

Wanuri Kahiu: Sanaa maridadi ya Kiafrika inayochekesha na kushangaza.

TED2017

Wanuri Kahiu: Sanaa maridadi ya Kiafrika inayochekesha na kushangaza.
894,360 views

Tumeshazoea hadithi za kutoka nje zikieleza Afrika kama sehemu ya vita, umasikini na uharibifu, anasema Wanuri Kahiu ambaye ni mwenza wa TED. Furaha ipo wapi? Anatambulisha "AfroBubbleGum" -- Sanaa ya Afrika ambayo inasisimua, yenye kufurahisha na isiyo na mjadala wa kisiasa. Kuwaza tena thamani ya mambo ambayo si makubwa. Kama anavyoelezea Kahiu kwa nini tunahitaji sanaa ambayo inagusa sehemu yote ya mapitio mwanadamu ili kuelezea hadithi za Afrika.

Jimmy Lin: Kipimo cha damu rahisi kinachoweza kugundua saratani mapema

TED2017

Jimmy Lin: Kipimo cha damu rahisi kinachoweza kugundua saratani mapema
1,471,238 views

Jimmy Lin anaendeleza teknolojia ya kugundua saratani miezi hadi miaka kabla ya njia zinazotumika sasa. Ametushirikisha mbinu za uvumbuzi huu ambazo huangalia viashiria vidogo vya saratani vinavyokuwepo kupitia kipimo rahisi cha damu, kugundua urudivu wa baadhi ya aina ya ugonjwa siku 100 mapema zaidi ya njia zilizo zoeleka. Unaweza kuwa mwali wa matumaini katika mapambano ambapo ugunduzi wa mapema huleta utofauti mkubwa.

David Miliband: Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu

TED2017

David Miliband: Mgogoro wa wakimbizi ni kipimo cha utu wetu
1,454,444 views

Watu millioni sitini na tano walitolewa katika makazi yao na migogoro na majanga katika mwaka 2016. Huu sio tu ni mgogoro; lakini pia ni kipimo cha kuwa sisi ni nani na tunasimamia nini, anasema David Miliband - kila moja wetu ana jukumu binafsi kutatua hali hii. Katika mazungumzo haya yenye umuhimu wa kipekee kuyaangalia , Miliband anatupa njia za dhahiri za kuwasaidia wakimbizi na kugeuza huruma na kuwawazia wengine kuwa vitendo.

Anne Lamott: Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi

TED2017

Anne Lamott: Ukweli 12 niliojifunza kupitia maisha na uandishi
5,458,934 views

Siku chache kabla ya kutimiza miaka 61, mwandishi Anne Lamott aliamua kuandika kuhusu kila kitu alichofahamu kwa hakika. Anazama katika mihangaiko ya mwanadamu anayeishi katika ulimwengu uliochanganika, wenye uzuri na hisia, unaompa hekima na ucheshi kuhusu familia, uandishi, maana ya Mungu, kifo na zaidi.

Sofi Tukker: "Awoo"

TEDNYC

Sofi Tukker: "Awoo"
1,670,035 views

Kundi la wanamuziki wawili wa Electro-pop linalofahamika kama Sofi Tukker likicheza na umati wa TED katika nyimbo yao ya mdundo wa haraka ya "Awoo", wakimshirikisha Betta Lemme.

Sitawa Wafula: Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa

TEDNairobi Ideas Search

Sitawa Wafula: Kwanini naongelea kuhusu kuishi na kifafa
891,685 views

Aliyewahi kubaki nyumbani kutokana na ugonjwa wa kifafa. Sitawa Wafula, ambae ni mhamasishaji wa afya ya akili alipata nguvu kuandika kuhusu ugonjwa wake. Kwa sasa, anahamasisha kwa ajili ya wengine ambao bado hawajatambua sauti zao, akivunja unyanyapaa na kutengwa katika kuongelea ni namna gani inavyokuwa kwa mtu anayeishi na ugonjwa wa kifafa.

Karim Abouelnaga: Shule ya kiangazi watakayo watoto

TED2017

Karim Abouelnaga: Shule ya kiangazi watakayo watoto
1,211,003 views

Kipindi cha kiangazi, watoto toka kaya maskini Marekani husahau karibu miezi mitatu ya walichosoma kipindi cha mwaka wa shule. Mjasiriamali wa elimu na Mshirika wa TED Karim Abouelnaga anataka kurekebisha upotevu huu wa elimu, kwa kubadili "anguko la kiangazi" kuwa fursa ya kwenda mbele na kukua kuelekea baadaye ing'arayo zaidi.

Stephanie Busari: Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli

TEDLagos Ideas Search

Stephanie Busari: Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli
1,358,172 views

Mnamo Aprili 14, 2014, shirika la kigaidi la Boko Haram liliteka zaidi ya wasichana wa shule 200 kutoka mji wa Chibok, Naijeria. Duniani kote, uhalifu huu ulifanywa mfano kwa kauli mbiu ya #BringBackOurGirls yaani "Rejesha Wasichana Wetu" -- lakini ndani ya Naijeria, maafisa wa serikali waliita uhalifu huu kuwa ni mzaha, kusababisha utata na kuchelewesha jitihada zozote za kuwakomboa wasichana hawa. Katika zungumzo hili shupavu, mwanahabari Stephanie Busari anaelekezea janga la Chibok kueleza hatari kubwa ya habari za uongo na nini tunaweza kufanya kuzizuia.

Todd Scott: Mwongozo wa Kifalaki wa kutumia difibrileta

TEDNYC

Todd Scott: Mwongozo wa Kifalaki wa kutumia difibrileta
1,149,314 views

Ikiwa Yoda atapata mshtuko wa moyo, utajua nini cha kufanya? Msanii na mkereketwa wa Huduma ya Kwanza Todd Scott anachambua kila kitu unachotakiwa kufahamu kuhusu kutumia AED, "Automated External Defibrillator", kwenye falaki hii na nyingine za mbali. Jiandae kuokoa maisha ya Jedi, Chewbacca (atahitaji kunyolewa kidogo kwanza) au mwingine yeyeote mwenye kuhitaji pamoja na dondoo zenye msaada. AED ni kifaa-tiba kinachotumia umeme kurudisha mapigo ya moyo katika mwendo wa kawaida

Sara Ramirez: "Rollercoaster" (Gari-bembea)

TED Talks Live

Sara Ramirez: "Rollercoaster" (Gari-bembea)
1,132,926 views

Mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na mwigizaji Sara Ramirez ni mwanamke mwenye vipaji vingi. Akiungana na Michael Pemberton kwenye gitaa, Ramireza anaimba juu ya fursa, hekima na kuinuka na kuporomoka kwenye maisha katika tamasha hili mubashara la wimbo wake, "Rollercoaster." Rollercoaster ni bembea mfano wa gari moshi ambayo reli yake inapanda juu sana na kushuka chini. Watu husikia raha wakati wa kupanda au ikiwa juu lakini huogofya wakati wa kushuka chini, kwani huwa kama yaanguka. Carousel ni bembea mfano wa farasi wanaokwenda wakizunguka duara. Farasi (au viti mfano wa kitu chochote) hufungwa kwenye kamba ipandayo na kushuka mithili ya mwendo wa farasi huku ikizunguka mduara.

Thordis Elva, Tom Stranger: Simulizi letu la ubakaji na maridhiano

TEDWomen 2016

Thordis Elva, Tom Stranger: Simulizi letu la ubakaji na maridhiano
5,570,439 views

Mwaka 1996, Elva Thordis alifurahia penzi la utotoni na Tom Stranger, mwanafunzi kutoka Australia. Baada ya sherehe ya Krismasi shuleni, Tom alimbaka Thordis, nahawakukutani baada ya miaka mingi. Katika majadiliano hayo ya ajabu, Elva na Stranger wanazungumzia miaka ya kuishi katika aibu na usiri, na kutualika kujadili changamoto ya hii kimataifa juu ya unyanyasaji wa kijinsia katika uaminifu mpya. Kwa mjadala, tembelea go.ted.com/thordisandtom.

Charity Wayua: Njia chache za kurekebisha Serikali

TED@IBM

Charity Wayua: Njia chache za kurekebisha Serikali
1,110,420 views

Charity Wayua aliweka ujuzi wake kama mtafiti wa kansa kwa mgonjwa asiyetarajiwa: Serikali ya nchi yake ya Kenya. Anaeleza jinsi yeye alisaidia serikali yake kwa kiasi kikubwa kuboresha mchakato wake kwa ajili ya kufungua biashara mpya, sehemu muhimu ya afya ya kiuchumi na ukuaji, na hivyo kusababisha miradi mipya na kutambuliwa na Benki ya Dunia kama mboreshaji mkuu.

Adam Grant: Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?

TED@IBM

Adam Grant: Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?
7,250,021 views

Katika kila mahali pa kazi, kuna aina tatu za msingi za watu: watoaji, wapokeaji na walipizaji. Mwanasaikoloji Adam Grant anazifafanua hizi nafsi tatu na anatoa mikakati ya kukuza utamaduni wa ukarimu na jinsi ya kuwaepuka wafanyakazi wabinafsi kuchukua zaidi kuliko sehemu yao.

Pico Iyer: Uzuri wa ambavyo hatutovijua

TEDSummit

Pico Iyer: Uzuri wa ambavyo hatutovijua
1,827,446 views

Takribani miaka 30 iliyopita,Pico Iyer alisafiri kwenda Japan, akaipenda nchi na akahamia huko. Mfwatiliaji wa karibu wa roho ya binadamu, Iyer anasema kwamba sasa anaona anajua machache kuhusiana na Japan -- au, hakika, kuhusu chochote kile -- kama ambavyo alidhani anajua miongo mitatu iliyopita. Kwenye hii tafakari ya kishairi kuhusu hekima, Iyer anaelezea kuhusu uelewa unavyokuja na umri: kadri tunavyodhani tunajua, ndivyo tunagundua tunajua kidogo.

Rebecca MacKinnon: Tunaweza kupambana na ugaidi bila kutoa kafara haki zetu

TEDSummit

Rebecca MacKinnon: Tunaweza kupambana na ugaidi bila kutoa kafara haki zetu
1,142,385 views

Tunaweza kupambana na ugaidi bila kuharibu demokrasia? Mwanaharakati wa Uhuru wa mtandao wa intaneti Rebecca MacKinnon anafikiri kwamba tutashindwa kwenye vita hii dhidi ya siasa kali na siasa za fujo ikiwa tutadhibiti mtandao wa intaneti na vyombo vya habari. Katika mazungumzo haya muhimu ametoa wito wa kusimama kidete kuhusu taarifa zilizodhibitiwa usiri na kuzitaka serikali kutumia njia bora kulinda, na sio kunyamazisha, waandishi wa habari na wanaharakati wanaopambana dhidi ya wenye siasa kali.

Ngozi Okonjo-Iweala: Jinsi gani Afrika itaendelea kukua

TEDSummit

Ngozi Okonjo-Iweala: Jinsi gani Afrika itaendelea kukua
918,971 views

Ukuaji wa Kiafrika ni harakati, sio ubabaishaji, anasema mchumi na aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala. Katika mazungumzo haya ya kusisimua yaliyo wazi,Okonjo Iweala anaelezea hatua endelevu barani na kuainia changamoto nane ambazo mataifa ya Kiafrika bado yanahitaji kuzungumzia ili kuweza kuwa na maisha bora baadaye.

Kang Lee: Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?

TED2016

Kang Lee: Unaweza kujua kweli kama mtoto anadanganya?
8,673,675 views

Je watoto hawadanganyi vizuri? Unafikiri unaweza kugundua uwongo wao kwa urahisi? Mtafiti wa maendeleo Kang Lee amechunguza nini kinatokea kisaikolojia kwa watoto wanapodanganya. Wanafanya mara nyingi kuanzia umri mdogo wa miaka miwili, na hakika wanafanya vizuri kweli. Lee anaelezea kwanini tusherehekee wakati watoto wanaanza kudanganya na kuwasilisha teknolojia mpya ya kugundua uwongo ambayo siku moja itaonyesha hisia zetu zilizojificha.

Jennifer Kahn: Ubadilishwaji wa Jeni sasa unaweza kubadili spishi nzima- milele

TED2016

Jennifer Kahn: Ubadilishwaji wa Jeni sasa unaweza kubadili spishi nzima- milele
1,922,129 views

Ubadilishaji jeni wa CRISPR unaruhusu wanasayansi kubadilisha mfumo wa DNA na kuthibitisha kwamba matokeo ya ubainishaji kijenetiki uliorekebishwa unarithiwa na vizazi vijavyo, na kufungua uwezekano wa kurekebisha spishi milele. Zaidi ya kitu chochote, teknolojia imepelekea maswali: Jinsi gani nguvu hii mpya itaathiri ubinadamu? Tutaitumia kubadilisha nini? Tumekuwa miungu sasa? Jiunge na mwandishi wa habari Jennifer Kahn anayejiuliza maswali haya na kuelezea ubadilishaji jeni: kutengenezwa kwa mbu wanaokinzana na magonjwa ambao wanaweza kutokomeza malaria na Zika.

Aditi Gupta: Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi

TEDxGatewayWomen

Aditi Gupta: Njia isiyo na mwiko kuongelea kuhusu siku za hedhi
1,676,262 views

Ni kweli: kuongelea kuhusu hedhi kunafanya watu wengi wakose raha. Na mwiko huo una matokeo yake: nchini India, wasichana watatu kati ya 10 hawajui hata hedhi ni nini wakati wa siku zao za kwanza, na masharti ya mila yanayohusiana na siku za hedhi yanaleta uharibifu kisaikolojia kwa wasichana. Kukua katika mwiko huu mwenyewe, Aditi Gupta alijua anataka kusaidia wasichana, wazazi, waalimu kuzungumzia kuhusu siku za hedhi kwa raha bila aibu. Anatushirikisha alivyofanya.

Casey Gerald: Injili ya mashaka

TED2016

Casey Gerald: Injili ya mashaka
2,123,426 views

Unafanyaje pale imani yako iliyosimama inageuka kua isiyo ya kweli? Pale dini ya Casey Gerald ilivyomuangusha, alitafuta kitu kipya cha kuamini - kwenye biashara, kwenye serikali, kwenye uhisani - lakini kukuta wakombozi wa uongo tu. Kwenye haya maongezi ya kuhamasisha, Gerald anatuhimiza tuulize imani zetu na kukubali mashaka yetu.

Alix Generous: Jinsi nilivyojifunza kuwasilisha maisha yangu nikiwa na Aspegaz

TEDWomen 2015

Alix Generous: Jinsi nilivyojifunza kuwasilisha maisha yangu nikiwa na Aspegaz
1,883,472 views

Alix Generous ni mwanamke mdogo mwenye maoni milioni na moja - amefanya sayansi ya kushinda tuzo, amesaidia kutengeneza teknolojia na anaongea kwa utani mzuri( utamuona). Ana Aspegaz, aina ya usonji unaoweza kuharibu ujuzi wa kawaida wa kijamii unaohitajika kuwasiliana, na amefanya kazi ngumu kwa miaka kujifunza namna ya kushirikisha mawazo yake kwa ulimwengu. Katika haya mazungumzo ya kufurahisha, ya kibinafsi, anaelezea hadithi yake - na maono yake kwa nyenzo itakayosaidia watu wengi kuwasilisha maoni yao makubwa.

Alaa Murabit: Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?

TEDWomen 2015

Alaa Murabit: Je dini yangu inasema nini hasa kuhusu wanawake?
3,804,611 views

Familia ya Alaa Murabit ilihamia Canada kutoka Libya alipokuwa na miaka 15. Kabala alijiona yuko sawa na kaka zake, lakini katika mazingira haya mapya alihisi vizuizi kuhusu yale mafanikio anayoweza kuyapata. Kama mwanamke wa Kiislam , alijiuliza kama haya kweli ni mafundisho ya dini? Kwa namna ya kuchangamsha anatushirikisha ugunduzi wa mifano ya viongozi wanawake katika historia ya imani yake - Na jinsi alivyoanzisha kampeni ya kupigania haki za wanawake kwa kutumia mistari ya Korani.

Memory Banda: Kilio cha shujaa dhidi ya ndoa za utotoni

TEDWomen 2015

Memory Banda: Kilio cha shujaa dhidi ya ndoa za utotoni
1,355,672 views

Maisha ya Memory Banda yalichukua njia ya tofauti na maisha ya dada yake. Dada yake alipovunja ungo, alipelekwa katika kambi ya awali ambayo inafundisha wasichana "jinsi ya kumridhisha mwanaume kimapenzi" Akapata uja uzito huko - akiwa na umri wa miaka 11. Lakini Banda akakataa kwenda. Badala yake , akaandaa wengine na akamuomba kiongozi wa jamii yake kupitisha sheria ndogo inayozuia wasichana kulazimishwa kuolewa kabla ya kufikisha miaka 18. Akaendeleza mapambano haya mpaka katika ngazi ya kitaifa ... akipata matokeo ya ajabu sana kwa wasichana wote , katika nchi yote ya Malawi.

Boniface Mwangi: Siku niliposimama peke yangu

TEDGlobal 2014

Boniface Mwangi: Siku niliposimama peke yangu
1,464,126 views

Mnasa picha Boniface Mwangi alitaka kupinga ufisadi nchini mwake Kenya. Hivyo aliweka mpango. Yeye na marafikize wangesimama na kupiga makelele kwenye mkutano wa hadhara. Lakini wakati huo ulipowadia…alisimama peke yake. Kilichotokea baadaye, anasimulia, kilimdhiririshia alikuwa mtu wa aina gani. Anavyosema, “Kuna siku mbili za umuhimu mkuu maishani mwako. Siku ya kuzaliwa, na siku utakavyogundua kwa nini." Picha za kuogofya.