TED Talks with Swahili transcript

Sir Martin Rees: Je tunaweza kuzuia mwisho wa Dunia?

TED2014

Sir Martin Rees: Je tunaweza kuzuia mwisho wa Dunia?
1,283,785 views

Baada ya mwisho wa dunia, binadamu hawapo, inaonekana kama kitu cha sayansi ya kubuniwa ya TV na filamu. Lakini katika maelezo haya mafupi na ya kushangaza, Lord Martin Rees anatuuliza tuwaze maafa yanayoweza kutukumba-- ya asili na ya kutengenezwa yanayoweza kufanya binadamu wote watoweke. Kama binadamu anayefuatilia vizuri yanayoendelea, anauliza: Ni kitu gani kibaya zaidi kinaweza kutokea?

Ziyah Gafic: Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha

TED2014

Ziyah Gafic: Vitu tutumiavyo kila siku, historia ya kusikitisha
1,040,925 views

Ziyah Gafic anapiga picha vitu tunavyotumia kila siku-saa, viatu, miwani. Lakini vitu hivi vinaonekana ni vya kawaida; vilifukuliwa kutoka katika makaburi ya watu waliokufa kutokana na vita ya Bosnia. Gafic, ambaye ni mshiriki wa TED na mkazi wa Sarajevo, amepiga picha kila kitu kilichotoka katika makaburi yale na kisha kutengeneza maktaba ya kudumu ya utambulisho wa watu waliofariki katika vita hivyo.

Clint Smith: The danger of silence

TED@NYC

Clint Smith: The danger of silence
5,033,082 views

"We spend so much time listening to the things people are saying that we rarely pay attention to the things they don't," says poet and teacher Clint Smith. A short, powerful piece from the heart, about finding the courage to speak up against ignorance and injustice.

Shai Reshef: Shahada ya gharama nafuu kabisa

TED2014

Shai Reshef: Shahada ya gharama nafuu kabisa
6,307,713 views

Katika chuo cha mtandaoni cha watu, yeyote aliyemaliza masomo ya sekondari anaweza akasoma masomo ya shahada ya usimamizi wa biashara au sayansi ya kompyuta - bila gharama za kawaida za ada (inagawa mitihani ina gharama zake). Mwanzilishi wake Shai Reshef anatumaini kuwa elimu ya juu inabadilika "kutoka kuwa upendeleo kwa wachache mpaka kuwa haki ya msingi , ambayo inapatikana kwa urahisi na unafuu."

Will Potter: Mpango wa Kustua wa kufanya maandamano na upinzani wa amani kuwa kosa la jinai.

TED2014

Will Potter: Mpango wa Kustua wa kufanya maandamano na upinzani wa amani kuwa kosa la jinai.
1,127,722 views

Mwaka 2002, Mwandishi wa habari za uchunguzi na TED Fellow Will Potter aliamua kupumzika kazi yake ya mara kwa mara ya kuandika kuhusu mauaji kwa ajili ya gazeti la Chicago Tribune. Alienda kulisaidia kundi linalofanya kampeni kinyume na matumizi ya wanyama katika majaribio ya kisayansi. "Nilifikiri itakuwa ni njia salama ya kufanya jambo jema," anasema . Lakini kinyume chake ,alikamatwa, na hapo ikaanza safari yake kwenye dunia ambayo maandamano ya amani yanaitwa ugaidi.

Ni kitu gani kinahitajika ili kuwa kiongozi bora

TED@BCG San Francisco

Ni kitu gani kinahitajika ili kuwa kiongozi bora
5,182,265 views

Kuna programu nyingi za uongozi siku hizi, kutoka mafunzo ya siku moja hadi katika mafunzo kwa ajili ya makampuni ya biashara. Kiukweli,hii haitasaidia. Katika hotuba hii ambayo ni makini na halisi ,Bibi Roselinde Torres anaeleza miaka yake 25 ya kuangalia na kutafuta viongozi bora makazini,na anashirikiana nasi haya maswali matatu muhimu ya viongozi wa makampuni kujiuliza ili kuweza kukua na kupata mafanikio.

Stephen Cave: Hadithi nne tunazoambia nafsi zetu kuhusu kifo

TEDxBratislava

Stephen Cave: Hadithi nne tunazoambia nafsi zetu kuhusu kifo
2,486,724 views

Mwanaphilosophia Steven Cave anaanza kwa swali lenye kazi lakini la kulazimisha kufikiria:Lini ulitambua utakuja kufa?Na cha kusisimua zaidi:Kwa nini wanadamu huwa tunakwepa kifo?Katika hotuba hii ya kuvutia Bwana Cave anachambua vitu vinne katika maisha ya binadamu ambapo huwa tunaambia nafsi zetu "ili kutusaidia kupambana na uoga wa kifo"

David Steindl-Rast: Unataka kuwa na furaha? Kuwa mtu wa Shukrani

TEDGlobal 2013

David Steindl-Rast: Unataka kuwa na furaha? Kuwa mtu wa Shukrani
7,468,760 views

Kitu kimoja ambacho binadamu wote tunacho pamoja ni kuwa na furaha,anasema kaka David Steindl-Rast,mtawa na mwanafunzi wa imani.Na furaha,anasema,inazaliwa kutoka katika shukrani.Somo linalohamasisha katika kwenda polepole,kuangalia unapokwenda,na kwa hayo yote,kuwa na shukrani.

Robin Nagle: Nilichokigundua katika uchafu wa Jiji la New York

TEDCity2.0

Robin Nagle: Nilichokigundua katika uchafu wa Jiji la New York
1,728,898 views

Wakazi wa Jiji la New York, wanatengeneza tani 11,000 za uchafu kila siku.Kila Siku! Takwimu hii ya ajabu ni moja ya sababu iliyomfanya Robin Nagle kufanya utafiti pamoja na idara ya usafi.Alipita njia zao,akaendesha mifagio ya umeme, na hata kuendesha gari la taka yeye mwenyewe- yote haya ili aweze kujibu swali linaloonekana kuwa rahisi lakini gumu: Ni nani anayetakiwa kusafisha baada yetu?

Sonia Shah: Sababu tatu kwa nini hatujaitokomeza  malaria

TEDGlobal 2013

Sonia Shah: Sababu tatu kwa nini hatujaitokomeza malaria
1,233,836 views

Tumejua jinsi ya kutibu malaria tangu 1600,kwanini ugonjwa huu bado unaua maelfu ya mamia kila mwaka?ni zaidi ya tatizo la kitabibu,anasema mwandishi wa habari Sonia Shah.Mtazamo wa historia ya malaria unaweka wazi sababu tatu kwanini ni ngumu kutokomeza malaria

Jack Andraka: Jack Andraka: Kipimo kinachotia matumaini cha kansa ya kongosho kutoka kwa kijana  mdogo.

TED2013

Jack Andraka: Jack Andraka: Kipimo kinachotia matumaini cha kansa ya kongosho kutoka kwa kijana mdogo.
4,827,010 views

Zaidi ya asilimia 85 ya kansa zote za kongosho zinagundulika kwa kuchelewa sana wakati nafasi ya kupona iko chini ya asilimia 2. Kwa nini iko hivi? Jack Andraka anaongelea jinsi alivyovumbua kipimo kinachotia matumaini cha kugundua kansa ya kongosho ambacho ni rahisi mno,kinafanya kazi kwa usahihi na hakihitaji kuingia katika mwili -- yote hayo kabla hata ya kutimiza miaka 16 ya kuzaliwa.

Angela Lee Duckworth: Angela Lee Duckworth:Ufunguo wa Mafanikio? Uvumilivu na Shauku.

TED Talks Education

Angela Lee Duckworth: Angela Lee Duckworth:Ufunguo wa Mafanikio? Uvumilivu na Shauku.
19,500,078 views

Akiacha kazi ya hali ya juu sana ya ushauri, Angela Lee Duckworth alianza kazi ya kuwafundisha hisabati wanafunzi wa darasa la saba katika shuke ya serikali jijini New York.Mara moja aligundua kuwa IQ haikuwa sababu pekee inayotoafautisha wanafunzi wanaofanya vizuri na wale wasiofanya vizuri. Hapa anaeleza nadharia yake ya uvumulivu na shauku katika kufanya vitu kama kiashiria cha mafanikio.

Ramsey Musallam: Ramsey Musallam: Sheria 3  za kuamsha kujifunza

TED Talks Education

Ramsey Musallam: Ramsey Musallam: Sheria 3 za kuamsha kujifunza
3,067,874 views

Ilihitajika hali ya kutishia maisha kumtoa mwalimu wa kemia Ramsey Musallam kutoka miaka kumi ya ufundishaji wa mazoea kuelewa kazi halisi ya mkufunzi: kupandikiza udadisi. katika mazungumzo haya ya kufurahisha na ya binafsi,Musallam anatoa sheria tatu za kuamsha tafakari na kujifunza, na kuwafanya wanafunzi kuwa na shauku jinsi dunia inavyofanya kazi.

Juan Enriquez: Maisha yako ya mtandaoni,ni ya kudumu kama mchoro

TED2013

Juan Enriquez: Maisha yako ya mtandaoni,ni ya kudumu kama mchoro
1,746,210 views

Kama je Andy Warhol alikosea na badala ya kua maarufu kwa dakika 15, hatujulikani tu kwa mda huo? Kwenye haya maongezi mafupi, Juan Enriquez anaangalia kwenye athari za kudumu za kushangaza za kushirikisha kidijitali siri zetu binafsi. Anashirikisha fahamu kutoka kwa Wanagiriki wa kongwe kutusaidia kushughulika na "michoro dijitali" yetu mipya.

Nilofer Merchant: Una Kikao?Fanya matembezi

TED2013

Nilofer Merchant: Una Kikao?Fanya matembezi
3,297,237 views

Nilofer Merchant ana ushauri mdogo ambao unaweza kuwa na mabadiliko makubwa katika maisha na afya yako:Wakati utakapokuwa na kikao kingine na mtu, kifanye kiwe ni "kikao cha matembezi" -- na yaache mawazo yazunguke wakati mnatembea na kuongea

Richard Turere:Uvumbuzi wangu ulioleta amani na Simba.

TED2013

Richard Turere:Uvumbuzi wangu ulioleta amani na Simba.
2,467,150 views

Katika jamii ya kimasai ambako anaishi kijana wa miaka 13,Richard Turere, Ng'ombe ni muhimu sana.Lakini mashambulizi ya simba yalikuwa yanaongezeka.katika maelezo haya mafupi ya kusisimua,mvumbuzi huyu mdogo anatushirikisha ufumbuzi wake unaotumia nguvu za jua ili kuwatisha simba.

Miguel Nicolelis: Nyani anayethibiti roboti akitumia fikra. Ukweli mtupu.

TEDMED 2012

Miguel Nicolelis: Nyani anayethibiti roboti akitumia fikra. Ukweli mtupu.
1,315,130 views

Tunaweza kutumia akili zetu kuthibiti mashine--bila kutumia mwili kama kiegezo? Miguel Nicolelis anazungumza kuhusu jaribio la kushangaza, ambalo nyani mwerevu huko Marekani alijifunza kuthibiti mashine, na pia mkono wa roboti huko Ujapani, kwa njia ya fikra tu. Jaribio hili lina athari kubwa kwa walemavu--na labda kwa sisi sote. (Filamu ilitengenezwa TEDMED 2012.)

Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji

TEDxSummit

Fahad Al-Attiya: Nchi isiyokuwa na maji
1,529,461 views

Fikiri kuhusu nchi ambayo ina umeme mwingi sana -- mafuta na gesi,Mwanga wa jua,upepo(na pesa) --lakini imepungukiwa na huduma muhimu kwa ajili ya maisha: Maji. Mhandisi wa miundo mbinu Fahad Al-Attiya anaongelea njia zisizotegemewa ambazo taifa dogo la Mashariki ya Kati la Qatar linatumia kutengeneza mfumo wake wa usambazaji wa maji.

Leslie Morgan Steiner:Kwa nini waathirika wa unyanyasaji majumbani hawaondoki

TEDxRainier

Leslie Morgan Steiner:Kwa nini waathirika wa unyanyasaji majumbani hawaondoki
5,800,883 views

Leslie Morgan Steiner alikuwa katika "penzi la wazimu" -- yaani, alimpenda sana mwanaume aliyemnyanyasa mara kwa mara na kumtishia maisha. Steiner anahadithia uhusiano wake, akisahihisha maoni potofu ya watu wengi kuhusiana na waathirika wa unyanyasaji wa majumbani , na kueleza vile wote tunavyoweza kumaliza kimya hicho. (Imerekodiwa katika TEDxRainier.)

Candy Chang: Kabla ya Kufa nataka...........

TEDGlobal 2012

Candy Chang: Kabla ya Kufa nataka...........
5,640,247 views

Katika eneo lake analoishi katika mji wa New Orleans,msanii na Mshirika wa TED ,Candy Chang aligeuza nyumba iliyotelekezwa na kuwa ubao mkubwa akiomba watu kuweka majibu yao katika swali: “Kabla ya kufa nataka ___.” Majibu ya majirani zake' -- yalishangaza, yalifurahisha -- na ikawa ni kioo kisichotegemewa cha jamii. (Jibu lako ni lipi?)

Hannah Fry: Maisha ni magumu kweli?

TEDxUCL

Hannah Fry: Maisha ni magumu kweli?
819,007 views

Kanuni zinaweza kutabiri eneo la mapinduzi yajayo? Kwenye haya maongezi mazuri, mwanahisabati Hannah Fry anaonyesha jinsi tabia tata za kijamii zinaweza kuchunguzwa na pengine kutabiriwa kupitia mifano ya ishara halisi, kama mitindo ya madoa ya chui au mgawanyo wa wawindaji na windo mbugani.

Damian Palin: Uchimbaji wa madini kutoka katika maji ya bahari

TED2012

Damian Palin: Uchimbaji wa madini kutoka katika maji ya bahari
1,002,297 views

Dunia inahitaji maji safi na salam, na mengi kati ya hayo kwa sasa tunayachukua kutoka baharini,tunayatoa chumvi na kuyanywa.Lakini tufanyeke na chumvi inayobaki nyuma? Katika mazungumzo haya mafupi ya kusisimua, Mshirika wa TED, Damian Palin anapendekeza wazo: Toa madini tunayoyahitaji katika chumvi hii inayobaki, kwa kusaidiwa na bacteria wanaokula metali

Hans Rosling: Dini na watoto

TEDxSummit

Hans Rosling: Dini na watoto
2,912,376 views

Hans Rosling alikua na swali: Kuna baadhi ya dini zenye kiwango cha juu cha uzazu zaidi ya nyingine -- na jinsi gani hii ina athiri ongezeko la idadi ya watu duniani? Akiongea kwenye TEDxSummit huko Doha, Qatar, alionyesha jedwali la takwimu kwa mda na katika dini. Akiwa na ishara yake ya ucheshi na ufahamu wa makini, Hans alifikia hatima ya kushangaza juu ya viwango vya uzazi duniani.

Chimamanda Ngozi Adichie: Chimamanda Adichie: Hatari ya simulizi moja

TEDGlobal 2009

Chimamanda Ngozi Adichie: Chimamanda Adichie: Hatari ya simulizi moja
21,248,547 views

Maisha yetu, tamaduni zetu, vimeumbwa na hadithi nyingi zinazoingiliana. Mwandishi wa riwaya Chimamanda Adichie anatoa simulizi ya jinsi alivyogundua sauti yake halisi kiutamaduni -- na anatahadharisha kwamba kama tukisikia hadithi moja juu ya mtu mwingine ama nchi nyingine, tupo hatarini kuelewa visivyo.

Al Gore warns on the latest climate trends

TED2009

Al Gore warns on the latest climate trends
952,886 views

At TED2009, Al Gore presents updated slides from around the globe to make the case that worrying climate trends are even worse than scientists predicted, and to make clear his stance on "clean coal."

Billy Graham akiongelea teknolojia,imani na mateso.

TED1998

Billy Graham akiongelea teknolojia,imani na mateso.
2,963,155 views

Akiongea katika mkutano wa TED mwaka 1998,Mchungaji Billy Graham anafurahia nguvu ya teknolojia kuboresha maisha na kubadilisha ulimwengu. -- lakini anasema kuisha kwa uovu ,mateso na kifo kutakuja tu ikiwa dunia itamkubali Kristo. Mazungumzo mahiri sana kutoka katika maktaba ya TED.

Mwaka wa kuishi Kibiblia wa A.J. Jacobs.

EG 2007

Mwaka wa kuishi Kibiblia wa A.J. Jacobs.
2,923,764 views

Akiongea katika mkutano wa hivi karibuni wa EG, mwandishi wa vitabu na habari na mwanafilosofia A.J. Jacobs anaongelea mwaka ambao aliishi akifuata maagizo ya Biblia katika kila eneo kadiri alivyoweza.